Maajabu katikati mwa kijiji: Askari kuwapiga wakazi wa CBD

1443171(2)
1443171(2)
Maajabu na mchezo wa kuigiza ulizuka baina ya askari na wakazi wa mji eneo la CBD.

Askari wa kaunti ya Nairobi wamewapiga wakazi wa eneo la CBD mjini Nairobi. Hii ni baada ya wakazi hao kumuokoa dereva mmoja wa tuktuk aliyekuwa akipinga kukamatwa na polisi.

"Walikuwa wakimkatili kwa mwanaume huyo mnyonge, kwanza walikivunja kioo cha tuktuk ile na kisha kumuangaisha. Tulipo simama kumsaidia walianza kupiga na rungu na pia kumpiga mwanamke aliyekuwa mjamzito," Alisimulia shaidi mmoja.

Mgogoro uliofanya wanabiashara na kutoendelea na biashara zao za kawaida nje ya chumba cha national archives.

Ilibidi askari wa GSU kuingilia kati ya mgogoro huo na kumsaidia mwananchi akiyekuwa anakamatwa na askari hao.

"Wakati polisi wa GSU waliingililia kati askari hao ambao walikuwa zaidi ya 10 waliweza kuenda na upande wa Odeon Cinema," Shaidi mwingine alisema.

Wakazi hao sasa wanataka gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko kuingililia katikati na uchunguzi kufanywa kisha askari hao kushtakiwa kwa dhuluma hiyo.

Afisa mkuu wa usalama wa kaunti ya Nairobi Tito Kilonzi aliambia gazetti la the star kuwa hakuwa amefahamu tukio hilo.

"Kama tukio hilo lilitendeka haijakuwa katika tahadhari yake na watauliza kwa askari aliyekuwa ameshika usukani," Alisema Tito.

Aliongezea na kusema kuwa maafisa wa ukaguzi mjini hawapaswi kuwadhuluma wananchi wasio na hatia bila kujali hali yao.

Sababu ya kutaka kumkamata mkazi huyo wa tuktuk haija bainika bado. Je ni vyema kuwapiga wananchi wasio kuwa na hatia ama wanapaswa kutatua tatizo hilo bila vita vyovyote?