Maandamano yazuka Kisii kabla ya ziara ya Ruto

Maandamano yamezuka huko Kisii kabla ya ziara ya Naibu wa rais  hivi leo .Maandamano ya  yamefanywa na makundi yanayounga mkono mchakato wa BBI  lakini wafuasi wa DP Ruto pia wamejitokeza kuyajibu kwa kufanyaa maandamano yao .

Ruto  anatarajiwa kuzuri eneo la Kisii  anapoendelea kuimarisha uungwaji mkono  kutoka kwa wakaazi wa kaunti hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 .

Ziara yake hiyo inajiri siku mbili baada ya Ruto kuanda mkutano na viongozi walioachaguliwa kutoka eneo hilo katika  makaazi yake rasmi mtaani Karen siku ya  jumatatu .

Ruto  anatarajiwa  kupokelewa na  viongozi wanaoendeleza kampeini zake katika eneo la Kisii  naibu wa gavana wa kaunti hiyo Joash Maangi  na mbunge wa mugirango kusini  Sylvanus Osoro .

Duru zaarifu kwamba Ruto anatarajiwa kufanya mkutano mwingine na viongozi wa jamii ya Gusii  baadaye  mwezi ujao