Mabingwa Liverpool waanza msimu vyema huku Mo Salah akifunga hat trick

IMG_20200913_095415
IMG_20200913_095415
Liverpool walianza utetezi wa ligi ya EPL kwa kuilaza Leeds 4-3 katika mechi ya kusisimua ugani Anfield.
Mo Salah alifunga magoli matatu na kuwahakikishia the Reds ushindi. Katika mechi ya kwanza msimu huu Arsenali ililaza Fulham 3-0 na kuchukua uongozi wa ligi huku Crystal Palace ikibwaga Southampton 1-0 nao Newcastle wakipiga Westham United 2-0.

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza kuwa Harry Maguire atasalia kuwa nahodha wa kikosi chake, licha ya kuandamwa na kesi ya kujaribu kuwahonga polisi na pia kukataa kutiwa nguvuni kwa kutumia nguvu kupita kiasi nchini Ugiriki.

Maguire alifungwa kwa miezi 21 na mahakama moja ya Ugiriki lakini alikata rufaa na kesi itaskizwa tena baadae mwaka huu.
Ligi ya Uhispania ilianza jana miezi miwili baada ya kukamilika, huku mechi tatu zikichezwa. Eibar ilitoka sare tasa na Celta Vigo, huku Granada ikinyanyua Athletic Bilbao 2-0 nao Cadiz ambao walipandishwa daraja msimu huu wakilazwa 2-0 na Osasuna.
Katika mechi za za La liga Valencia itacheza na Levante, huku Villarreal ikipiga dhidi ya Huesca nao Valadolid wakicheza na Real Sociedad.
Mbali na hayo kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone  amepatikana na virusi vya Corona na atasalia karantini kwa siku 14. Muajentina huyo hakuonyesha dalili zozote lakini atakuwa chini ya uangalizi kwa wiki mbili. Atletico Madrid watakabana koo na Granada katika mechi ya ufunguzi wa msimu wa La Liga mnamo tarehe 21 Septemba.