Machachari sio kipindi tena, Inspekta Mwala na Papa Shirandula kufanyiwa mageuzi

Govi wa Machachari amefunguka mwanzo mwisho kuweka mambo sawa kuhusu taarifa za kipindi chao kukatishwa runinga ya Citizen

Malik Lemuel almaarufu kama Govi amesimulia kuwa baadhi ya waigizaji waliacha shoo hiyo Januari.

Shoo ya Machachari ilikatishwa kwa misingi kwamba umri wa waigizaji haukuenda sawa na maudhui ya kipindi hiki.

"Kuna taarifa kuwa umri wetu ulikuwa umeizidi shoo...'

Soma hadithi nyingine;

'Msisikilize upuzi kama huo. Ukweli ni kuwa shoo haipo na hatufeel vizuri ila ni sawa tu..."

"Kilicho na mwanzo kina mwisho..." Alisema Govi

Zipo habari kwamba shoo hii haikuenda sawia na hadhira lengwa.

"Watu wengi wanataka kujua sababu za kukatishwa kwa shoo ya Machachari..."

'Ila sijui cha kusema kwa sababu niliacha Januari...'

'Ilikuwa ndoto yangu ya utotoni...'

Meneja anayezalisha vipindi Stanley Ngige  alisema kuwa,

Soma hadithi nyingine;

" Kipindi hiki hakikuwa kinaenda sawa na hadhira lengwa. Kizuri na ambacho tungefanya ni kukatisha shoo hiyo na kuanzisha 'Johari'...."

"Tulifanya kila jitihada za kuongea na hawa vijana ili waweze kukubali matokeo..."

Vipindi ya Papa Shirandula, Tahidi High vinatarajiwa kufuata mkondo ule.

Shoo ya Papa Shirandula itafunikwa na Maria katika mchakato wa kuona vipindi vipya vimeanza kuruka.

Vipindi kama Inspekta Mwala, Papa Shirandula, Mother-In-Law vinatarajiwa kufanyiwa mabadiliko makubwa.