Machifu waonywa dhidi ya kuitisha hongo ili kusajili wanafunzi Maskini kunufaika na fedha za CDF

wana
wana
Wanafunzi elfu moja mia moja hamsini na mbili kutoka vyuo vya anuwai, vyo vikuu na shule za upili na za msingi kutoka eneo bunge la Kabuchai kaunti ya Bungoma wana kila sababu ya kutabasuimau baada ya mbunge wa eneo hilo James Lusweti kuwapa fedha kutoka CDF za kuwawezesha kulipa karo.

Lusweti akizungumza katika afisi za CDF eneo la Msese hii leo amesema kwamba wanafunzi wa vyuo vya anuwai na vikuu watapokea shilingi milioni nane huku wale wa shule za msingi na upili wakipokea shilingi milioni tano.

Mbunge huyo amewatahadahrisha wazazi na wakaazi dhidi ya kutapeliwa na machifu kutoa hongo ili waweze kunufaika na fedha hizo akionya kwamba shule atakayepatikana atachukuliwa hatua kali za kisheria.

-Brian Ojamaa