Rais wa Urusi Vladimir Putin huenda ameanza kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba anasalia madarakani hata baada ya kipindi chake kuhudumu kutamatika mwaka wa 2024. Putin ambaye mbinu zake za kusalia uongozini zimezua sifa na lalama kutoka kwa wafuasi na wakosoaji wake ,amependekeza mageuzi makubwa ya kikatiba hatua iliyoifanya serikali nzima ya waziri mkuu Dimitri Medvedev kujiuzulu siku ya jumatano.
Saa 24 baada ya hotuba ya Putin kuhusu mpango wa kurekebisha katiba na mfumo wa uongozi wa urusi , Mikhail Mishustin aliyependekezwa kuwa waziri mkuu mpya ameidhinishwa na bunge la taifa hilo .
Mishustin alipata kura 383 kati ya 424 zilizopigwa bila pingamizi na wabunge 41 wakijipeusha na kura hiyo. Kupandishwa cheo kwa Mishustin ni sehemu ya mageuzi yaliyotangazwa jana na Putin ambapo amepnedekeza rais kupewa maamlaka zaidi ya kuwezesha kuwafuta kazi maafisa wasiotekeleza kazi zao ipasavyo.