Machungu ya corona! Kenya airways yataka mkopo kutoka kwa serikali kufanikisha shughuli zake

KQ-Plane
KQ-Plane
Shirika la ndege nchini Kenya Airways ambalo kwa sasa linasafirisha mizigo hadi mataifa ya kigeni limeitaka serikali kulipa shilingi bilioni 4 ili kufanikisha safari zake kutokana na hasara kubwa iliyosababishwa na corona.

Kulingana na mwenyekiti wa KQ Micheal joseph, shirikaa hilo lilikuwa limetuma maombi ya kupewa shilingi bilioni 9 mnamo Januari na kufikia sasa, wamepokea shilingi bilioni 5 ili kufufua.

Joseph anasema anatarajia kupokea mgao wa mkopo huo kwa awamu ya pili kufikia Juni mosi ili kufanikisha mahitaji ya kila mfanyakazi huku shughuli kama za shirika hilo zikitarajiwa kurejelewa hivi karibuni.

“We’ve been grounded for almost three months now. During that time, we’ve maintained all of our 38 aircrafts. We have to pay leases and meet insurance costs which do not go away whether you fly or not,” amesema Joseph.

KQ imeandikisha hasara kubwa baada ya shughuli zake nyingi kusitisha kutokana na  janga la Corona ambalo lilifanya mataifa mengi kusitisha shughuli za ndege kama njia ya kupunguza usambaaji wa virusi hivyo hatari.