Madaktari wa Tanzania hawataki kuja Kenya

Chama cha Madaktari nchini Tanzania kimepinga mpango wa kuwatuma madaktari 500  humu nchini wakisema Tanzania ina upungufu mkubwa wa madaktari.

Hii inafuatia makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Kenya mwishoni mwa wiki ambapo madaktari wapatao 500 watapata ajira nchini Kenya.

chama hicho pia kimeelezea hofu kuhusu usalama wa madaktari hao kwani kuna pingamizi kutoka kwa  viongozi wa upinzani kuhusu mpango huo.