Madereva 9 ni miongoni mwa wale waliopatikana na corona – Aman

Shinikizo zinazidi kutolewa kwa serikali kuangazia mipaka yake na taifa jirani la Tanzania baada ya madereva tisa waliosafiri kutoka taifa hilo kupatina na virusi vya corona .

Aman alisema kuwa madereva hao walikuwa wameingia nchini wakitumia mpaka wa Namanga unaounganisha Kenya na Tanzania katika kaunti ya Kajiado, hali ambayo imewatia kiwewe wakaazi wa Kajiado.

Akitoa tangazo hilo, katibu Aman alisema kuwa uwezekano wa kufunga mipaka ya Kenya upo na ni jambo ambalo serikali inapania kuangazia.

“On the issue of closing the border, every possibility is on the table and up for discussion and when the time comes and it is necessary, that measure will be taken,” Aman alisema.

Miongoni mwa kaunti zingine ambazo zinapakana na taifa la Tanzania na zimeathirika pakubwa na ongezeko la watu walioambukizwa virusi hivyo na wanaotokea taifa jirani la Tanzania ni, Kaunti ya Wajir, Mandera na Migori.

Hatua hiyo sasa imefanya serikali kupendekeza kuwa kila mkenya kifanyiwa vipimo vya corona kabla ya kulazwa katika hospitali yoyote ile nchini.