Madhara ya Corona! Ajax hawatatawazwa mabingwa wa ligi ya Uholanzi

NA NICKSON TOSI

"Hatua ya shirikisho la soko nchini  la kutotawaza timu yetu ya Ajax taji msimu huu ni ya kueleweka.." Amesema meneja wa timu Edwin Van der Sa baada ya ligi kuu ya Uholanzi kutupiliwa mbali kutokana na corona.

Ajax walikuwa wanaongoza katika jedwali la ligi hiyo huku mechi 9 zikisalia kutamatisha ligi hiyo msimu huu.

Mabingwa hao wa zamani wa Uropa sasa watakosa la msimu huu baada ya serikali kuongeza masharti ya kutotaka watu kukusanyika katika maeneo ya umma hadi septemba Mosi.

Ni mara ya kwanza sasa tangu 1945 tangu ligi ya Uholanzi kukosa bingwa .

Ajax aidha watafuzu kwa michezo ya ligi za mabingwa msimu ujao huku wapinzani wao wa karibu AZ Alkmaar wakitarajia kucheza michezo ya mjujo ndiposa kujipatia tiketi ya champions league.