Madhara ya pombe! Msamaria mwema ajitokeza kuwasaidia jamaa wanaokunywa vitakasa mikono

EYXEnOMWkAA4oBz
EYXEnOMWkAA4oBz
Baada ya taarifa kushamiri katika mitandao ya kijamii kuhusiana na jamaa watano ambao wamekuwa wakinywa vitakasa mikono almaarufu kama hand sanitizers eneo la Mathioya kaunti ya Murang'a, msamaria mwema kwa jina Stanley Kamau wa shirika la Ahdai Kenya amejitokeza na kusema atawasaidi jamaa hao.

Kamau amesema atatumia hela zake kuwapeleka jamaa hao walioathirika na unywaji wa pombe katika kituo cha kubadili tabia yaani Rehab ili wapewe ushauri nasaha.

Kutokana na hatua ya serikali kuongeze vigezo kwa wamiliki wa mikahawa na hata vilabu, halaiki ya watu waliokuwa na mazoea ya kunya vileo wamejipata katika njia panda kwani asilimia kubwa ya maeneo hayo yangali mahame na hayajafunguliwa.

Aidha masharti ya kuonya watu kutangamana katika eneo moja zaidi ya watu 15 imechangia watu wengi waliokuwa wamezoea kunya pombe kuwa katika njia panda kwani maagizo hayo yamekuwa magumu kwa asilimia kubwa ya vilabu nchini kuyatimiza.