Madini Classic azungumzia Chuchuma ya Willy Paul, sababu za kutoipa shavu

Screenshot_20190523_1739202__1570177312_91262
Screenshot_20190523_1739202__1570177312_91262
Katika mahojiano ya simu na kitengo cha Papa Na Mastaa, staa wa muziki Madini Classic amefunguka mwanzo mwisho kuhusu swala wa Willy Paul kutomhusisha katika kuipa nguvu na kuipigia upatu nyimbo ya Chuchuma.

Staa huyu amesema kuwa Willy Paul kutomhusisha katika kuipa nguvu Chuchuma sio kwamba hapendi ngoma hiyo,

Haya yanajiri huku ngoma hiyo ikionekana kufanya vizuri katika mitandao ya kijamii na YouTube.

“Ile ngoma binafsi naipenda sana . Lakini ukiona zile clips Willy Paul alikuwa anatafuta msanii na kumuambia vile anafaa kuifanya.”

https://www.instagram.com/p/B2_cltSpGAZ/

Soma hadithi nyingine;

“Mimi kutoifanya sio kwamba siipendi au kwamba hakunimind.’

Madini alikuwa anazungumza katika kitengo cha Phone Call Ya Rais akidokeza haya yote.

Aidha, Madini hakusita kuzungumzia nyimbo iliyofungiwa ya Wamlambez. Staa huyu haoni sababu ya wimbo huu kufungiwa.

Soma hadithi nyingine;

‘Ni ile nilichagua mwenyewe nikaona mbona generation ya leo wanasikiliza Wamlambez sana mi nikaona nidondoshe hii.”

“Wamlambez ndo aina ya ngoma zetu sasa ndo maana zinashabikiwa.”

Madini pia amemzungumzia Noble Mirror92 msanii ambaye amemshirikisha katika ngoma hii.

“Huyo ni kama kakangu wa kitambo. Ni ile mtu nimeshinda nikimuona kutoka kitambo. Halafu kingine ni rapa mzuri kiukweli so kipaji kwanza.”