Madrid iko tayari kuipatia Man United £90m pamoja na Gareth Bale

Real Madrid iko tayari kuipatia Manchester United £90m pamoja na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 30, ili kumsajili Paul Pogba, lakini inataka mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 kuimarisha kiwango chake cha mchezo uwanjani . (El Desmarque, in Spanish)

Real Madrid ina mpango wa kumuuza mshambuliaji Bale na kiungo wa Colombia James Rodriguez 28 ili kupata fedha za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylina Mbappe 20. (Calciomercato).

Wakati huohuo, rais wa Real Madrid Florentino Perez ana mpango wa kufanya kila kitu katika uwezo wake ili kumnyakua Mbappe katika uwanja wa Bernabeau msimu ujao. (AS)

Washauri wa kiungo wakati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, wanajaribu kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani kuhamia katika ligi ya MLS. (Mail)

Hatahivyo imeripotiwa kwamba Ozil amejiandaa kuendelea kuichezea Arsenal kwa muda mrefu. (Star)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kwamba wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz ,21, ambaye alijiunga na Aston Villa msimu huu. (Manchester Evening News)

Bayern Munich inafikiria uhamisho wa mwezi Januari wa beki wa Atletico Bilbao na Uhispania Unai Nunez na wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye pia anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal na Everton. (Goal.com)

-BBC