Maelfu ya vijana wasio na kazi Nairobi kuanza kupata senti 616 kila siku

jobpic
jobpic

NA NICKSON TOSI

Zaidi ya vijana alfu 10,000 wanaoishi jijini Nairobi wataanza kupata shilingi 616 kila siku kutokana na mradi wa serikali wa kazi mtaani unaolenga kuajiri vijana ambao hawana ajira majira haya ambapo taifa linakabiliana na Corona.

Huu ni mpango ulioanzishwa na idara ya miundomsingi ya Nyumba, 'State Department of housing', ambao ulianzishwa kote katika mitaa yote 23 nchini kama njia ya kubuni nafasi za ajira kwa vijana zaidi ya 26,000.

Katika jiji kuu la Nairobi, vijana wanaoishi kwenye mitaa ya Kibra, Mathare, Mukuru na Korogocho wamesajiliwa katika mpango huo ambapo watatarajiwa kusafisha miji na maeneo mengine.

Katibu Charles Hinga amesema kuwa vijana hao watajukumika kufanya usafi kama vile kuosha miji, kufukizia dawa, kuzoa taka, kukata vichaka na kufungua mifereji ya kupitisha maji taka.