Maeneo 5 ambayo unaweza ukapatana na kipenzi cha maisha yako

Wakati unapotaka sana kupatana na mtu ambaye labda mtachumbiana na kufunga ndoa mara nyingi huwa ni ngumu kwa wengine wetu kufanikiwa. Wengine huamua kutafuta mitandaoni na wengine hata kwenye maeneo ya burudani.

Kama bado hujafanikiwa huenda ukapatana na mchumba wako katika mojawapo ya maeneo haya.

1. Kanisani

Hili si Jambo la kigeni hata hivyo. Kuna baadhi ya watu ambao walijiunga na makanisa fulani bila hata nia ya kumpata mchumba lakini mambo yakawa tofauti. Iwapo hujawahi kujaribu kutafuta mapenzi kanisani basi jaribu bahati yako. Huenda ukampata yule mume au mke ambaye umekuwa ukimsubiria.

2. Harusini

Ni dhahiri kwa unapoalikwa harusni umealikwa ili uweze kusherehekea ndoa ya pengine jamaa au rafiki yako. Na hakuna makosa yeyote iwapo utaamua kuchukua fursa hiyo kutizima iwapo kuna binti au kijana ambaye labda amekupendeza na mkachumbiana naye. Katika harusi kila mtu anasherehekea na kuwa na wakati mzuri na hali hii inaunda mazingira kamili ya wewe kujaribu bahati yako na ukibahatika utaondoka katika sherehe hiyo na mpenzi wa maisha.

3. Kwenye Matatu

Kuna wachumba ambao tushaskia wakisimulia hadithi ya jinsi walivyopatana na si nadra siku hizi kuwasikia wakisema walipatana kwenye matatu. Kwa hivyo wakati mwingine unapoabiri gari na umeketi kando ya mwanadada ambaye amekuzuzua, jaribu bahati yako. Jitolee hata kumlipia nauli angalau na hadithi yenu huenda ikaanzia hapo.

4. Katika klabu

Baadhi yetu tumeshikilia dhana kwamba huwezi kukutana na mtu mwenye tabia nzuru ama ambaye huenda akawa mume au mke wako kwenye vilabu, lakini si kweli. Si kila mtu ambaye huende katika maeneo y burudani ana tabia potofu. Kwa hivyo hata pale kwenye klabu unaweza kupatana na atakayekuwa kipenzi cha maisha yako.

5. Ofisini

Pia ofisini ama popotepale unapofanya kazi unaweza kumpata mume au mke wako wa siku za usoni. Mwanadada, kama kuna jamaa ambaye amekupendeza pale ofisini jaribu bahati yako pia, i lazima yeye aje kwa wa kwanza. Fungua roho yako, mueleze hisia zako, labda mapenzi yatakuzwa hapo.

Vile vile unaweza kupatana na mtu ambaye mtachumbiana popote pale, si lazima iweka kati ya maeneo haya. Kwa hivyo wakati mwingine unapoalikwa harusini ama mkutano wa kirafiki ama upo popote pale kuwa makini usijaukapitwa na baraka zako.