Magavana sasa waitaka serikali kuidhinisha kaunti zilizoathirika na mafuriko na nzige kwenye mipango yake

Magavana sasa wameirai serikali kuidhinisha kaunti ambazo zimeathirika na mafuriko na nzige nchini katika mikakati yake ya kufungua uchumi wa taifa.

Mwenyekiti wa jopo la magavana hao Wyclife Oparanya amesema anapania kukutana na rais Kenyatta ili kujadili swala hilo kuhusiana na kaunti hizo zilizoathirika pakubwa.

Kwa sasa, serikali inaangazia uwezekano wa kufungua uchumi wa taifa baada ya janga la corona kuathiri pakubwa shilingi ya Kenya kwenye soko la hisa.

Hatua ya kufungwa kwa mikahawa, baa na hata kupiga watu maarufu kumechangia pakubwa uchumi wa taifa kudorora.

Huku serikali ikipania kuchukua hatua hiyo, Oparanya amehoji kuwa majimbo yaliyotatizika na mafuriko na mlipuko wa nzige ni sharti yaangaziwe katika mikakati hiyo mipya ya serikali.

Kufiki sasa, watu 237 wameaga dunia kutokana na mafuriko huku familia 161,000 zikiachwa bila makao baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.

"As the Council of Governors, we support the President's plan to come up with a post-coronavirus economic plan to bring the country's ailing economy back on track after overcoming the pandemic but the floods menace should be part of the strategy,"  amesemaOparanya.

Oparanaya amesema kuwa mafuriko yameharibu chakula kilichokuwa kimepandwa na wakulima na kuwaacha maelfu ya watu yakiwa bila makao, jambo ambalo amesema ni sharti serikali iliangazie haraka.

"Kenyans affected by calamities should be factored in the strategy for an all-round recovery plan,' amesema Oparanya.

Kutokana na mafuriko hayo, Oparanya amesema wakulima hawatakuwa na cha kuvuna msimu huu kwani mazao yao yote yameharibiwa na mafuriko.