Mageuzi ya Katiba yanukia! Kenyatta asema ipo haja ya kufanyia marekebisho katiba

EZa4tl3WkAAM-MO.jfif
EZa4tl3WkAAM-MO.jfif
Rais Uhuru Kenyatta amezungumzia umuhimu wa kufanya marekebisho ya katiba ya kenya ya 2010 akisema kuna baadhi ya vipengele ambavyo ni lazima vifanyiwe marekebisho ili kuafikia umoja zaidi nchini.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Madaraka yaliyokuwa yanafanyika kwenye Ikulu jijini Nairobi, Kenyatta amesema ni kufanyia tu baadhi ya vipengee marekebisho bali si kuibadili Katiba yenyewe.

"...It is not a moment to replace it but to improve it. A moment that will correct what we did not get right in 2010," amesema Kenyatta.

Amesema taifa la Kenya linahitaji baadhi ya vipingee ambavyo vitaleta umoja miongoni mwa wananchi na taifa kwa jumla.

 "We need one that will bring an end to cycles of violence that we have witnessed since 1992. One that will deepen our democratic credentials and lead to an  inclusive society," aliongezea Kenyatta.

Uhuru amesema taifa haliwezi kuafikia malengo yake iwapo marekebisho hayo hayatafanyika kwa Katiba.

"If we have done great things. The. We must not be afraid to change the system if it does not help us do this," amesema Uhuru.

Amesema azimio la kuifanyia marekebisho katiba ya mwaka 2010 ni kutokana na usemi wa mwanasiasa wa zamani humu nchini Tom Mboya kuwa Katiba haiwezi kuwa ndio kila kitu iwapo haijazaa matunda yake kwa wananchi.

"He argued that a Constitution cannot be useful to a country if it is an end to itself. A good Constitution must be responsive to the aspirations of a nation & be a means to a greater end," amesema Kiongozi wa taifa.

Mapema naibu rais Wiliiam Ruto alimhakikishia rais Kenyatta kuwa wakenya wanaliombea taifa kutokana na virusi vya corona ambavyo vimekithiri nchini.