Magix Enga ajitenga na madai ya kampuni inayodai mgao kwa wimbo mpya wa Tanasha

89939704_202004667813056_564283604561349954_n
89939704_202004667813056_564283604561349954_n
Producer wa Kenya Magix Enga kwa mara nyingine tena amejitenga na madai ya kampuni moja ya humu nchini inayodai mgao wa fedha katika wimbo mpya wa Tanasha Donna Sawa.

Kampuni hiyo Hexacorp Limited inadai kuwa ilikuwa imetoa kibali cha wimbo huo kwake kwenye mitandao ya Youtube kwa niaba ya Magix japo mzalishaji huyo amejitenga na madai hayo.

Katika ujumbe alioutuma kwenye Instagram, Magix amesema kuwa hana uhusiano wowote na kampuni hiyo na hana uwezo ama hisani yoyote katika wimbo huo wa Tanasha.

"My attention (has been) drawn to the fact that a certain company named Hexacorp has claimed rights of the Sawa song by @tanashadonna on my behalf under her YouTube. I wish to state that I am not associated with and have not engaged this company to manage my rights and I do not have any rights in the song," aliandika.

Aliongezea kuwa kampuni hiyo ilikuwa inatekeleza wizi kwa kudai ilikuwa inamwakilisha na kutaka iliondoe jina lake na kukoma kutumia ufuasi wa watu wengine ili kujiendeleza.

"Taking someone's rights to their work is theft and pretending to represent someone is fraud. Hexacorp keep my name out of your scam and stop messing with the work of hardworking artists," Magix .

Maajuzi Magix aligonga vichwa vya habari baada ya kudai kuwa rapper wa Amerika Tekashi 6ix9ine alitumia baadhi ya sauti yake katika wimbo wake Gooba.

Matamshi hayo yalifanya wimbo huo kuondolewa kwenye Youtube kwa siku kadhaa baada ya Magix kuripoti madai hayo.