Mkutano huo utafanyika katika taasisi ya kustawishaji mtaala wa elimu na utajadili tena suala tata la kufunguliwa kwa shule wakati huu wa janga la corona .
Mwezi julai ,wizara ya elimu ilitangaza kwamba huenda shule hazitafunguliwa hadi januri mwaka ujao . Magoha hata hivyo amesema uamuzi huo unaweza kubadilishwa kulingana na jinsi kenya inavyokabiliana na janga la virusi vya corona .
Katika wiki moja iliyopita kumekuwa na ongezeko la wito wa kufunguliwa kwa shule huku wanaomiliki shule za kibinafsi wakiitaka serikali kuzingatia kuzifungua shule mapema kuliko ilivyokuwa imetangaza hapo awali .
Hatua hiyo imetokana na kupungua kabisa kwa visa vya Covid 19 vinavyoripotiwa kila siku huku watu wengi pia wakipona ugonjwa huo na kurejelewa kwa shughuli za kawaida katika sekta nyingi za uchumi .
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutoa mwongozo mpya mwishoni mwa mwezi huu kama sehemu ya mikakati ya kufungua uchumi ambao umelamazwa na janga hilo tangu mwezi machi mwaka huu .
Mnamo agosti tarehe 25 mzazi mmoja aliwasilisha kesi kortini akitaka kuishurutisha wizara ya elimu kuzifungua shule .
Shule zilifungwa mwezi machi wakati Kenya ilipothibitisha kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa corona .
Mwenyekiti wa muungano wa wamiliki wa shule za kibinafsi Mutheu Kasanga amesema wanapinga pendekezo la kuwataka watahiniwa kurudia madarasa kwa mwaka mzima .