Mahakama kutoa amri mwili wa mwanamke mmoja kufukuliwa kwa uchunguzi

Mahakama ya juu ilitoa amri kuwa mwili wa mwalimu mwanamke mji wa Eldoret kufukuliwa ili kufanya uchunguzi zaidi kilicho sababisha kifo chake.

Mahakama hiyo ya Eldoret ilitoa amri hiyo ili kufanya uchunguzi zaidi kilicho sababisha kifo chake, ya mwalimu aliye kufa mwaka jana Desemba.

Jaji Hellen Omondi alisema ufukuaji wa mwili huo wa Veronica Kwamboka Kemunto ni nia ya haki na kuwezesha uchunguzi wa DCI.

Omondi alisema kuwa mwili huo uweze kufukuliwa mbele ya kila mtu na kulingana na maelekezo ya polisi.

"Si kwa mgogoro wa jamii kwa maana wengine wao hawakurithishwa na uchunguzi wa maiti na wanataka maoni ya pili,"Alizungumza Omondi.

Wana jamii wa Veronica wanataka mwili huo kufukuliwa kwa upasuaji wa pili lakini mume wake Elija Oginda aliweza kupinga maoni hapo na kusema kuwa hataki mwili huo kufukuliwa.

Alisema kuwa kati ya sababu zingine kufukuliwa kwa mwili huo kutafanya ashikwe na kiwewe lakini Omondi alimwambia kuwa jitihada  za haki hupea kipaumbele hisia katika jambo hilo.

Jaji huyo alikataa rufaa za Elija dhidi ya kufukuliwa kwa mwili huo. Kemunto alikufa Desemba 11 mwaka jana na kuzikwa Desemba 21 katika mji wa Eldoret.

Wanajamii wengine waliambia mahakama mwili huo uweze kufukuliwa kwa madai kuwa madoa ya damu yalipatikana katika chumba chake cha kulala.

Wdwin Oginga ambaye ni mtoto wake aliambia mahakama kuwa alishuku upasuaji uliofanywa na William Nalianya katika hospitali ya rufaa ya Moi.

Madoa ya damu ambayo yalipatikana chumbani mwake mwalimu huyo, yaliweza kufanya familia yake kuenda mahakamani ili mwili huo uweze kufukuliwa kwa ajili ya uchunguzi mpya kilicho sababisha kifo chake.

"Madoa ya damu ambayo tuliyapata katika chumba chake cha kulalam ndio kilisababisha tuhuma zetu na kutaka mwili huo kufukuliwa kwa uchunguzi mpya na kujua kilicho sababisha kifo chake," Edwin alieliza.

Lakini babayake Elijah aliweza kutofautiana na familia hiyo kuwa mwili wa mke wake usifukuliwe kwa sababu alirithika na upasuaji wa kwanza uliofanywa.

Kulingana na upasuaji uliofanywa na daktari Nalianya unasema kuwa marehemu alikufa kwa sababu ya tatizo za moyo.

Oginda aliweza kuongezea na kusema kuwa alirithishwa na matokeo ya kwanza kuwa mke wake alikufia hospitalini bali si kwa nyumba ,lakini jaji Omondi alisema upasuaji wa kwanza haukuweza kueleza kwa kina kilicho sababisha marehemu huyo kushindwa na kali za moyo.

Huku ikisababisha tuhuma katika familia, Oginda na Edwin waliweza kutoa ushaidi wao mbele ya jaji Omondi ambaye amekuwa akiskiza rufaa ya Oginda kuhusu mwili huo kufukuliwa.

Amri ya kufukua mwili huo iliweza kutolewa na hakimu mkuu Naomi Wairimu mnamo Januari 10, kufuatia kesi iliofaili na dadake marehemu Truphena Osinde kupitia kwa DCI.

Kupitia kwa DCI katika ripoti iliofikishwa mahakamani imeunga mkono mwili huo uweze kufukuliwa na uchunguzi kufanywa mbele ya kila pande.

Kupitia kwa wakili wake Morris Kimuli alisema kuwa ripoti za upasuaji zilizoletwa mbele ya mahakama familia ilishuku kwa sana.

Elija mume wa marehemu ambaye amewakilishwa na wakili Dennis Magare alikataa madai kuwa mke wake alifariki akiwa nyumbani na kusema mke wake alifariki akiwa hospitalini mjini Eldoret.

Aliweza kusisitiza kuwa kufukuliwa kwa mwili huo si sawa na haifai. Magare alisema baada ya utawala wa mahakama na amri ya mahakama waweza kuwa katika ufukuaji wa mwili huo.

Jaji alitoa amri mwili huo kufukuliwa kwa haraka iwezekanavyo mara moja polisi wakitayarisha utaratibu.