KARIUKI

Mahakama yakosoa DCI kwa kumkamata bwenyenye, Humphrey Kariuki

Mahakama ya Milimani imekosoa hatua ya DCI kumkamata bwenyenye Humphrey Kariuki akiwa bado katika majengo ya mahakama.

KARIUKI
“Nilikuwa awali nimetoa agizo la kutokamatwa kwa Humphrey Kariuki na angejiwasilisha mwenyewe kwa afisi za DCI,” Hakimu mkuu Francis Andayi alisema.

 
Kariuki alitiwa mbaroni tena siku ya Jumatatu katika majengo ya mahakama ya milimani punde tu baada ya kuachiliwa na Andayi kwa dhamana ya shilingi milioni 11 kuhusiana na tuhuma za kukwepa kulipa ushuru wa takriban shilingi bilioni 41.

Kitany amvua nguo seneta Linturi, hakamani

Alimatwa tena kwa madai ya kuwa na kemikali aina ya ethanol.Akizungumza na “The Star” siku ya Alhamis, wakili Danstan Omari alisema kwamba afisa yeyote wa polisi hakubaliwi kumkamata mshukiwa katika eneo hilo la mahakama.

 
“Kulingana na sheria, bunge, mahakama, maeneo ya kuabudu, taasisi za elimu na viwanja vya ndege ni mahali ambamo mtu hafai kushikiwa,” alisema.

Gavana Samboja adinda kupatanishwa na waakilishi wadi

Wakili aliongeza kwamba kuna kinga katika mahakama kwa sababu ni eneo linalolinda haki muhimu za kila mmoja na kwamba kila mtu katika maeneo ya mahakama yuko chini ya ulinzi wa idara hiyo. Hakimu kwa hivyo, alisema kukamatwa tena kwa mfanyibiashara huyo kulikuwa matumizi mabaya ya mamlaka ya polisi.

 
“Kwa hivyo sitaruhusu polisi kumkamata yeyote katika majengo ya mahakama,” Andayi alisema.

Photo Credits: The star

Read More:

Comments

comments