Mahakama yakubali mzee kibor kufanyia wanawe DNA

Kibor
Kibor
Mfanyabiashara kutoka Eldoret Mzee Jackson Kibor ni rasmi kuwa anaweza kuwafanyia wanawe vipimo vya DNA kuhusiana na mzozo wa ardhi yenye ekari 2000.

Mahakama imemtakja Kibor kufanyia wanawe hao sita vipimo hivyo kabla ya kuanza kuwapa kipande hicho cha ardhi.

Kulingana na Kibor hakuwa amemwoa mama mzazi wa watoto hao na anashuku kuwa huenda kuna vile anapanaia kuwatumia kama njia ya kuwapa ardhi hiyo.Kibor vile vile anashuku kuwa huenda si watoto wake halisi.

Kibor amewakashifu watoto wao kwa kujaribu kuuza shamba hilo kama walivyokuwa wamefanyia baadhi ya biashara zake zilizoko kaunti za Nairobi na Mombasa.

“Hawa watoto yangu ni wakora…wakora kwa sababu waliuza nyumba yangu Karen, Nairobi, na wakauze ingine Nyali, Mombasa,” amesema  Mzee Kibor.

“Hawa watoto wanasumbua, nitawapeleka DNA nihakikishe kama ni wangu ama si wangu kwa sababu mimi sikuoa mama yao.”

Mzee Kibor pia amesema anahofia maisha akiitaka serikali kurudisha bunduki yake ili kujilinda yeye mwenyewe.

“Hawa watoto wanaweza piga mimi kwa sababu bado wanataka hii shamba..serikali irudishie mimi silaha yangu nijilinde,” alisema Kibor.

Mzee Kibor amesema kuwa sasa amelazimika kuipa serikali ekari 10 za ardhi ili kujenga vituo vya polisi.