Mahakama yampa OCS wa Kamukunji wiki mbili kuhakikisha mshukiwa aliyetoroka amepatikana

OCS
OCS
Mkuu wa kituo cha polisi cha Kamukunji Shamir Yunis amepewa wiki mbli na mahakama ya kuhakikisha kuwa mshukiwa wa Uganda aliyetoroka katika kituo hicho amepatikana. Mshukiwa Martin Wasike na wengine walikuwa wanakumbwa na mashtaka ya kumteka nyara polisi.

Yunis akiwa mbele ya mahakama hiyo ya Nairobi amesema mshukiwa kimiujiza tu alihepa kutoka ndani ya kizimba ambacho alikiuwa amezuiliwa Mei 14 asubuhi.

Aliongeza kuwa maafisa wa Ujasusi walikuwa wametuma habari kwa vituo vingine kuvifahamisha dhidi ya tukio hilo.

Aliomba mahakama iwape muda wa kufanya uchunguzi akisema kuwa kila mwanadamu hukosea maishani.

“man is to error, that’s a fact of life. One of us must have erred and if it was deliberate then the institution is dealing with the issue, we are asking the court so that we see if the resorts we’ve put in place bear fruits.” Alisema Yunis

Hakimu Kennedy Cheruiyot katika maamuzi yake aliamwambia mkuu huyo wa kituo cha Kamukunji kuwa aendeleze uchunguzi wa haraka kwani taarifa kuhusiana na kutoweka kwa afisa wa polisi bado hazijabainika wazi.

Mahakama ilisema kuwa washukiwa hao Wasike, Shariff  Wanabwa na Phoebe Anindo walimteka nyara afisa huyo wa polisi mnamo Januari 19 mwaka huu.

“…on or about January 19, 2020 at an unknown place within the Republic of Kenya, jointly with others not before court kidnapped police constable Abel Misati in order that the said officer may be murdered or disposed of as to be put in danger of being murdered,” taarifa ya hakimu.

Mahaka imetenga mashahidi 10 kutokana na kesi hiyo