Mahakama yamtaka Kinoti kufika mbele yake

Mahakama mjini Kiambu imemtaka mkurugenzi mkuu wa jinai DCI George Kinoti kufika mbele yake baada ya kukiuka agizo lililotolewa na mahakama moja Nairobi la kutaka kuachiliwa kwa magari mawili ya Rashid Echasa.

Maagizo hayo yaliyotolewa Ijumaa, yamemtaka Kinoti kufika mbele yake Julai 3.

“You are hereby required to attend this court at 8pm on July 3, 2020 in the above case to explain why you have not released motor vehicle as ordered by the court in the above case and remain in attendance until released,” 

Hakimu mkuu Stella Atembo Juni 10, alitoa uamuzi kuwa magari yaliyokuwa yamezuiliwa ya Echesa aina ya Toyota Lexus, Ford Ranger na Merceds Benz yalikuwa yanazuiliwa kinyume na sheria.

“The act of detaining property without any support or any law of order of the court with sufficient reasons contravenes the constitution which provides for the right to private property and opportunity to be heard,”  Stella Atembo.

Mahakama pia ilibaini kuwa magari hayo matatu hayakuwa miongoni mwa masharti yaliyotolewa na mahakama ya kuanzisha uchunguzi.

Maafisa kutoka DCI yalitwaa magari matano kutoka kwa Echesa mnamo Machi 2 mwaka huu baada ya mkaazi mmoja kutoka kaunti ya Kisumu kufikisha lalama zake kwa DCI akisema alikuwa amelaghaiwa magari hayo.