Maina Kamanda shaking hands with WilliamRuto

Ruto hafai kuwa rais wa Kenya, Maina Kamanda asisitiza

 

Mbunge maalum Maina Kamanda amesema kwamba wakenya hawafai kuanza kujijazia mengi kuhusiana na salamu zake na naibu rais William Ruto na kudhani kwamba amebadili mawazo yake kumhusu.

 

Maina Kamanda shaking hands with WilliamRuto
Maina Kamanda akisalimiana na naibu rais WilliamRuto

Siku ya Alhamisi, Kamanda alikuwa miongoni mwa kundi la wabunge walioandamana na naibu rais William Ruto kwa hafla ya ukumbusho wa kifo cha mwanzilishi wa taifa la Kenya Hayati mzee Jomo Kenyatta. Picha za wawili hao wakisalimia wakiwa na furaha ziliacha wakenya vinywa wazi.

 

Akizumgumza katika eneo la Ol Kalou Jumamosi jioni, mbunge huyo alisema kwamba hakuandamana na Ruto bali Ruto alimpata katika eneo la kaburi la mzee Kenyatta na kwamba salamu zao hazijabadilisha msimamo wake kuwa Naibu Rais hastahili kuwa rais wa Kenya kwa sababu mbali mbali.

Mbunge huyo pia aliwahimiza wakenya kujitokeza kwa wingi kwa zoezi la kuhesabu watu linaloendelea kote nchini.

Alitoa wito kufanyika kwa zoezi lenye uazi huku akitilia shaka zoezi la mwaka 2009.

 

Read here for more

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments