Maisha yalinilazimisha kuhamia kwa nyanyangu na watoto 4 - Edward

Mwanamume ameiambia mahakama kwamba yeye pamoja na watoto wake wanne wanamtegemea nyanya yake wa miaka 90 pamoja na kwa chakula na malazi kwani hakuwa na mahali pa kwenda.

Edward Mwiti alimweleza hakimu mkuu wa korti ya jiji la Nairobi Roslyne Oganyo kuwa shida ilianza hapo nyuma baada ya baba yake kuonyesha upendo kwa mama yake na kumuacha yeye ateseke.

"Simjui babangu mzazi, lakini nikiwa mchanga mamangu alipendana na mwanaume ambaye alimpenda yeye pekee lakini aliyenikataa hadharani." alisema.
Alisema kuwa pindi tu mamake alianza kuishi na babake wa kambo alilazimishwa kutoka nyumbani na kulelewa na nyanyake, Jennifer Kailentu katika kaunti ya Meru.
Mwiti aliiambia korti kuwa baadaye alimuoa Salome Kinya lakini ndoa hiyo haikudumu kwani walitengana mwaka wa 2012 akimuacha na watoto wanne.
"Mheshimiwa, nilioa lakini baadaye tulitengana na mke wangu kwa sababu ya maswala ya ndoa, alinikimbia, basi nililazimika kurudi nyumbani nyanyangu na watoto wanne."
He futher told court that the diffrences he had with his wife were irreconciliable. Baadaye aliiambia mahakama kwamba tofauti alizokuwa nazo na mkewe hazingeweza kuleta maridhiano kati yao.
Mwiti alikuwa akizungumza katika kesi ambayo anashtakiwa kwa utupaji wa taka katika barabara ya Ladhis, Nairobi kinyume na sheria Novemba 5.
Alikubali mashtaka hayo.
Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama kwamba alikamatwa wakati askari wa Jiji walikuwa kwenye doria yao ya kawaida katika eneo hilo.
Hakimu alimshauri amtongoze tena mke wake ili waweze kuungana tena kwani yeye na watoto wake wanne ni mzigo mkubwa kwa nyanya yao.

Hakimu alimpa kifungo cha majaribio cha miezi sita.

-Corazon Wafula