Maiti ya mwanaolimpiki aliyeripotiwa kupotea yapatikana

radio africa
radio africa
Mwili wa Blanca Fernandez ambaye ni mshindi wa medali katika olimpiki huko uhispaniola, umepatikana mlimani karibu na mtaa wa Madrid.

Fernandez aliripotiwa kupotea mnamo agosti tarehe ishirini na tatu mwaka huu. Polisi wamebaini baada ya uchunguzi kuwa Fernandez aliondoka nyumbani kwake bila simu na gari lake lilionekana mwisho mtaani Madrid.

Fernandez alikuwa mwanamke mhispaniola wa kwanza kushinda taji la medali katika mashindano ya olimpiki. Fernandez ameaga dunia akiwa na miaka 56.