‘Majambazi waliwabaka mamangu na dadazangu nikishuhudia’ Jamaa asimulia

Masks
Masks
Kama kuna  masaibu ambayo watu huogopa zaidi maishani ni kukumbana na majambazi au wahalifu .

Kuna n visa vya watu wengi ambao wameuawa au kuachwa na majaraha  mabay hata kupewa ulemavu na majambazi lakini aliopitia Thomas Shikoti  wakati majambazi walipovamia boma lao mwaka wa 2015 sio jamhbo litakalosahalika katika fikra zake hadi leo .

Kando na kuwaibia kimabavu pesa walizokuwa wamepata baada ya kuuzwa miwa , Thomas  alilazimishwa kuangalia kisa kizima wakati majangili hao walipomshika na kumbaka mamake na dadazake wawili mbele yake huku babake pia akilazimishwa kushuhudia ukatili huo . Familia nzima iliachwa na majonzi na kumbukumbu za tukio hilo kila siku huleta machozi  kwa watu wote wa familia yao .

Hadi leo anashangaa mbona haingetosha kwa majambazi hao kuchukua tu pesa ambazo babake alikuwa amelipwa na kmapuni moja ya sukari kwa miwa aliouza . Kwa jumla  majmbazi hao walitoroka na shilingi laki saba ambazo familia yake ilikuwa imepanga kununua kipande cha ardhi . Uchunguzi wa polisi hadi leo haujawahi kuwapa haki na hatua hiyo imewafanya kukosa imani kabisa na mfumo wa sheria  nchini . Kwa ajili ni watu wachache wa familia waliojua kuhusu malipo ya fedha hizo kwa babake Thomas , familia hiyo inashuku njama ya kuwaibia na kuwatendea unyama mamake na dadake zake huenda ilipangwa na mmoja wa watu wa familia yao .

Kando na kuchukua pesa zote  ambazo babake alikuwa amelipwa ,majambazi hao pia  walibeba kila walihoweza kuweka katika  walilokuja nalo na kilichowahofisha majirani kuwasaidia usiku huo ni kwamba majambazi wote sita walikuwa wamejihami kwa bunduki na wengine walikuwa wamevalia sare za polisi. Kumekuwa na uvumi kwamba huenda baadhi yao walikuwa kutoka taifa jirani la Uganda lakini haiwezekani mtu kutoka Uganda anaweza kupanga njama ya kufanya unyama huo katika eneo la Kakamega bila usaidizi wa washirika wake upande sa Kenya .

Thomas  anasema hasira yake hata  sio kwa sababu ya mali walioibiwa usiku huo bali kinachomwakaza moyo hadi leo na kimekataa kujifutakatika kumbukumbu zake ni unyama wa kuwabaka mamake na dadake akiona .Hilo kamwe amesema hatowahi kuwasamehe watu hao na uchunguzi wake binafsi kuhusu  mtu  wa familia aliyepanga njama hiyo umemfanya kung’amua mambo ya kushtusha kwa sababu hakujua wivu wa ndani  katika familia yao ungeweza kuwfanya jamaa zake kushirikiana na majambazi ili kuwasababishia majonzi kwa njia hiyo .