Majibu Nayo! Tazama jinsi Raila Odinga Junior alivyorusha ‘kombora’ twitter

Mwanawe kiongozi wa ODM Raila Odinga Junior  jana amempiga mmoja wa watumizi wa twitter  kumbo kali sana pale twitter alipojaribu kutilia doa kiwango cha masomo yake . Jamaa huyo Joseph Omondi alijutia mbona alianzisha vita hivyo na Junior kwani jibu lake sio lililotarajiwa .

Wengi wa wanaotumia twitter wanbafahamu kwamba mfalame wa majibu makali huwa   wakili Miguna Miguna lakini huenda anapata ushindani kutoka kwa Raila Junior . Hata hivyo wengi wa waliofuatilia majibizano hayo kati ya Omondi na Raila Junior walionekana kughadhabishwa na jibu ambalo Junior alilitoa wakisema kama mtoto wa  Raila Odinga ,alifaa kuonyesha  ustaarabu kidogo mtandaoni .

https://twitter.com/Railajunior/status/1228883044863479809

Katika majibizano hayo Omondi alikuwa akieleza kwamba mwanawe Naibu wa rais  June Ruto ana kisomo zaidi ya Raila Junior na hivyo basi anastahili kushikilia nafasi  anayohudumu  kama mwakilishi wa balozi huko Poland .Hata hivyo majibu ya RailaJunior yalimuacha kila mtu kinywa wazi .