Jina Mkanyageni ni la mtaa mmoja eneo la Old Town mjini Mombasa na kwa ufahamu wako pengine utafikiria linamaanisha kukanyaga mtu. Lakini mtaalamu wa historia ya Pwani, Stambuli Abdulahi Nassir anasema jina hili linamaanisha - mtu anayekanya wageni au kitu kigeni, ndio huuitwa mkanya geni.
Nassir anasema baadi ya majina kama Dungo Kundu , Steji ya Paka yamekua yakidhaniwa kuwa na asili lakini ukweli ni kwamba hayakuvumbuiwa kitambo .
Jina kama Toa Tugawe, watakwambia ni mtaa ambao ulikua na wezi wengi kwa hivyo ukitoka safari zako na ukutane nao , baso watakwambia utoe ulicho nacho ili mgawanye.
Mtongwe ni kivuko kila mmoja anakifahamu sana. Lakini kwa mujibu wa Nassir hili sio jina moja bali mawili, Mto-Ngwe. Huu ulikua mto mdogo sana [mto] ambao kipimo chake kilikua kikipimika [ngwe].
Haya ni baadhi tu ya majina ya maeneo katika eneo hili, Dunge Unuse, Kadongo, Milango Saba, Floringi, Kadzandani, Mbuzi wengi na mengine mengi.
Je unafahamu majina ya ajabu katika eneo lako na asili yake? Yataje.