'Majivu yake yalitawanywa ufukoni Diani,' Mjane wa Bob Collymore aeleza kwa nini walichagua Diani

Ni takriban mwaka mmoja tangu aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Safaricom Bob Collymore aage dunia, mjane wake alifichua kuwa majivu yake yalisafirishwa hadi pwani ya Diani Mjini Mombasa kwa maana alikuwa anapapenda sana kuzuru eneo hilo. Akiwa kwenye mahojiano Bob Collymore alifichua haya;

"BOB’S ASHES WERE DEPOSITED INTO THE SEA IN DIANI. DIANI WAS HIS FAVOURITE BEACH IN THE WHOLE WORLD, SO WE THOUGHT IT BEST TO PUT HIS ASHES IN THE SEA THERE.

SO THAT NO MATTER WHERE ANY OF US, HIS FAMILY OR FRIENDS, ARE IN THE WORLD, AS LONG AS YOU ARE NEAR OR OUT AT SEA, THEN YOU ARE IN THE PRESENCE OF WHERE HIS REMAINS ARE." Alizungumza mkewe Bob.

Collymore alipatikana na maradhi ya saratani ya damu mwaka wa 2017 katika hospitali moja mjini London na kuhamishiwa katika Nairobi Hospital kwa matibabu zaidi. Marehemu alifahamisha runinga ya citizen mwaka wa 2018 kuhusu hali yake ya kiafya na kuelezea vile hali yake ilikuwa inaimarika.

Wakati alipopatikana na saratani hiyo madaktari walimwambia kwamba alikuwa ameishi na hali hiyo mwilini mwake kwa muda wa miezi sita. Alipata dalili za ugonjwa huo alipokuwa nchini Morocco baada ya kuhisi kuwa na homa. Pia alikuwa na maumivu kwenye mifupa yake.

“I FINALLY WENT TO A DOCTOR HERE IN NAIROBI WHO SAID I THINK YOU ARE VITAMIN D DEFICIENT. I WILL GIVE YOU SUPPLEMENTS ." Alisema Collymore.

Alienda katika hospitali ya Nairobi alipopimwa damu mara thelathini, ugonjwa huo ulisababisha mwili wake kutotoa seli nyeupe za damu zilizosababisha mwil kutokuwa na kinga dhidi ya maradhi. Alitakiwa kufanyiwa matibabu kwa muda wa miezi tisa, mwishowe Collymore alikaa hospitalini kwa muda wa miezi tisa na wiki mbili.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO