Majonzi ! Safaricom yabadilisha rangi ya kurasa za Facebook, Twitter na Insta

Baada ya kifo cha mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom kuaga dunia. Rangi ya kurasa za mitandao za kampuni zimebadilishwa rangi yake ya kawaida na kuwa na rangi ya kijivu ghafla. Hii ni ishara kuwa wanaomboleza kiongozi wao.

Soma hapa :

Tazama hapa:

Kifo cha ghafla cha Bob Collymore kimewashagaza wengi nchini. Bosi wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom Bob Collymore ameiaga dunia leo asubuhi. Kulingana na taarifa rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa  Safaricom Nicholas Nganaga, Collymore alifariki mapema siku ya Jumatatu akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu.

Soma hapa pia:

Bob Collymore amekua akiugua saratani na amekua akipokea matibabu tangu Oktoba mwaka uliopita. Amemwacha mke na watoto wanne.

Kwa mujibu wa habari kutoka Safaricom, Collymore amekuwa akipokea matibabu kwa hospitali kadhaa na hivi majuzi amekuwa akitibiwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi.