Majumba yaliyojengwa kwenye ardhi za umma kubomolewa Taita Taveta

Mwakilishi wa wadi ya kaloleni katika kaunti ya Taita Taveta Omar Ahmed amesema kuwa kaunti hiyo itaanza kubomoa majengo yote ambayo yamejengwa kwenye ardhi za umma.

Omar amefichua kuwa kwa sasa kuna miradi kadha ya kusaidia jamii inayofaa kuanzishwa katika maeneo mbali mbali ila ardhi zenyewe zimenyakuliwa na mabwenyeye.

Anasema wamiliki wa majumba hayo watapewa notisi ya kuondoka katika ardhi hizo ili kupa nafasi kwa miradi ya serikali kuendelea.