Makachero wa DCI wamkamata wakili aliyejaribu kutoa hongo kwa afisa wa uchunguzi

Wapelelezi kutoka idara ya uchunguzi wa jinai(DCI) katika mtaa wa Kasarani wameemkamata wakili Anthony Kirunyu Karoki kwa kujaribu kumpa hongo afisa wa polisi wa uchunguzi kwa usalama wa watuhumiwa wtano waliotiwa mbaroni mnamo tarehe 12 Agosti.

Kulingana na DCI Karoki alikuwa na shillingi 1,000 na imewekwa kama ushahidi na maonyesho huku akingoja kufikishwa mahakamani.

Watuhumiwa hao ambao wakili wao alijaribu kupeana hongo walikamatawa na laini za simu 1,200 ambazo zimesajiliwa na hazijasajili na vifaa vya elekroniki.

Pia DCI ilisema kuwa watani hao walikuwa wametayarishwa kuenda kortini ambapo Karoki alijaribu kutoa hongo kwa afisa wa uchunguzi.

Kupitia kwenye ukurasa wa twitter idara hiyo iliandika ujumbe huu;

" Bwana Anthony Kirunyu Karoki ambaye anafanya mazoezi ya utetezi katika idara ya Karoki.co advocate amekamatwa hii leo na maafisa wa upelelezi wa DCI Kasarani

Hii ni kufuatia kwa kutoa hongo kwa afisa wa uchunguzi kwa shillingi 900,000 kwa usalama wa watuhumiwa watano waliokamatwa na vifaa vya elekroniki

Watano hao walikamatwa mnamo Agosi 12,2020 na laini za simu 1200 ambazo zimesajiliwa na zingine hazijasajiliwa na simu za elekroniki ammbapo walikamatwa

Shillingi 1000 alizopatikana nazo katika madhehebu hayo ilirekodiwa na idara ya DCI na kuwekwa kama onyesho wakati wa kuskizwa kwa kesi yake

Pia atatuhumiwa kwa kuvunja sheria za utetezi katika tena No.46 ya mwaka wa 2016." DCI Iliandika.