Makachero wa DCI wamnasa mshukiwa wa wizi aliyevunja gari Mombasa

Makachero wa DCI wamemnasa mmoja wa wahusika wa wizi uliofanyika Mombasa na kuwaacha wanamtandao kinywa wazi. Kamera za CCTV zilirekodi jinsi kundi hilo la wahalifu lilivyopanga njama yao ya kuvunja gari moja na kuiba mkoba unaoaminika kuwa na pesa au bidhaa zingine zenye dhamana.

Ni video ambayo ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii huku wanamitandao wakishangazwa na wizi huo.

Polisi walisema mshukiwa mmoja kwa jina Boris Mutua alikamatwa nyumbani kwake eneo la Kiembeni na wengine wanasakwa.

Polisi walipata gari ambalo lilitumika kwenye wizi huo na kutambua lilikuwa limetundikwa nambari za usajili feki wakati wa kisa hicho.

"Baada ya kupata taraifa kutoka kwa umma, kikosi cha makachero kikiongozwa na CCIO Mombasa kimemkamata Boris Mutua Malai kutoka nyumbani kwake eneo la Kiembeni." Ilisoma taarifa ya DCI.

Kile hawakujua ni kuwa kundi hilo lilikuwa limetumia ujanja na kuweka nambari zingine feki juu ili wasitambuliwe haraka.

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1307547036334592013

"Tuliweza kupata gari aina ya Toyota Ractis lenye usajili KCX 726Q. gari hilo lilinaswa na kamera Septemba 17 na nambari KCU 113P katika eneo la kisa hicho kwenye jumba la Texas karibu na Cinemax eneo la Nyali."

Walijaribu kwa mara kadhaa kufungua milango yake na lilipokataa wakaingia kwenye gari lao na kutoka na kifaa butu. Mmoja wao aligonga dirisha la nyuma na kupasuka akapata nafasi ya kufungua mlango wa nyuma upande wa kulia.