Makahaba wafurushwa Msumbiji kwa kupuzilia masharti ya serikali

SEX-WORKER
SEX-WORKER
Taifa la Msumbiji ama Mozambique kama linavyojulikana limewafurusha makahaba 43 kutoka nchini humu baada ya kukiuka amri za serikali za kutaka watu wasitangamane maeneo mbali mbali ili kupunguza kuenea kwa virusi vya corona.

Miongoni mwa makahaba hao baadhi yao walikuwa wanatoka mataifa ya Zambia na Zimbabwe ambao walitiwa mbaroni wakiwa kwa shughuli ya kawaida,.

Kufikia sasa taifa hilo limewatia watu 109 mbaroni kwa kukosa kufuata maagizo ya serikali katika mji wa Beira.

Kati ya watu 109,watu 43 walikuwa ni makahaba wa mataifa ya kigeni ambao walifungishwa virago na kurejeshwa kwa mataifa yao.

Kufikia sasa taifa la Msumbiji limesajili visa 227 vya maambukizi ya virusi vya corona ,watu 12 wakiwa wanatoka katika vitongoji vya Sofala.
Rais wa taifa hilo Filipe Nyusi aliongezea makataa ya watu kutotoka nje hadi Aprili mwaka huu.