Makahaba Wanataka Kutambuliwa Na Serikali

picha: AFP | 

Makahaba wanataka kutambuliwa na serikali ili waruhisiwe kuendesha shughuli zao pasi kusumbuliwa kila mara.

Doty Agala kutoka muungano wa makahaba nchini anasema kwamba kazi yao ni kama tu kazi yoyote ile nchini Kenya na inafaa kuheshimiwa.

Ukahaba ni marufuku nchini na hii si mara ya kwanza kukuwa na muito wa kazi hiyo kuhalalishwa.

Katika mwaka wa 2012, aliyekuwa meya wa jiji la Nairobi wakati huo, George Aladwa, alipendekeza kupitishwa kwa sheria ambayo itahalalisha ukahaba katika jiji la Nairobi lakini hata hivyo juhudi hiyo ulipingwa vikali.

Sheria za ukahaba zinatofautiana kutoka kwa nchi moja hadi nyingine na baadhi ya nchi ambazo zimehalalisha ukahaba dunia ni Uholanzi, Ujerumani, Ugiriki, Benin, Armenia, Uingereza na Zambia.