Makali ya COVID 19: Makahaba wachangiwa shilingi 49,000 kununua chakula na kulipa kodi ya nyumba wakati huu wa janga ka corona

makahaba
makahaba
Wasamaria wema na wahisani wametoa mchango wa  takribana shilingi elfu 50 ili kuwasaidia makahaba kununua chakula na kulipa kodi za nyuma wakati huu wa janga la corona  na kulipia  faini za kuachiliwa huru walipokamatwa na polisi kwa kujihusisha na shughuli zao.

Watu 16 wamechangisha shilingi  49,490.

Hazina hiyo iliundwa mwezi aprili na  muungano wa  kuwasaidia wanawake wanaojishughulisha na biashara hiyo  (Keswa)  ambao hutetea pia maslahi ya wanaofanya ukahaba.

Kafyu  imesababisha kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali zinazoathiri shughuli za makahaba na hivyo basi kubana njia zao za kujipa kipato

"Wateja wengi wamezuiwa dhidi ya kuingia katika madanguro na wengi hawataki kuonekana mchana’ Shirika la Keswa limesema.

“ Sekta ya uchukuzi   pia imezidisha nauli wakati huu wa janga la corona na kufanya kuwa vigumu kwa wanaofanya kazi za ukahaba kusafiri hadi kliniki za gharama ya chini kwa matibabu’

Wengi wao wameshindwa kupata pesa za  kutibu  maradhi yanayowakumba yatokanayo na virusi vya HIV na hivyo basi kuhatarisha maisha yao huku wengine wakifurushwa kutoka nyumba za kukodi kwa kushindwa kulipia.

Muungano huo amesema makahaba hutegema sana sekta ya jua kali kupata mapato na kuathiriwa kwa sekta hiyo pia kumevuruga shughuli zao .