fred-compressed

Makali ya Matiang’i: Maafisa wawili wasimamishwa kazi kwa madai ya ufisadi

Waziri wa usalama wa ndani Fred  Matiang’í amesema kuhusu kusimamishwa kwa maafisa wawili katika idara ya usajili wa watu kwa madai ya kashfa za ufisadi.

Waziri Matiang’i pamoja na katibu mkuu Karanja Kibicho wamekuwa wakipiga kambi katika eneo hilo lililoko katika jumba la ACK Bishop, Upper Hill katika juhudi za kupunguza msongamano na kuhakisha kwamba huduma katika afisi hizo zinatekelezwa ipasavyo.

‘Nitamsamehe Kwa Kuvua Nguo Iwapo Ataomba Msamaha,’ Jamaa Aambia Mahakama

Matiangi alisema kuwa ziara zake za kila siku katika idara hiyo ya CRB ilitokana na malalamishi mengi kutoka kwa umma kuhusu kucheleshwa kwa vyeti vya kuzaliwa.

“Tumekuwa hapa tangu juma lililopita ikiwemo wikendi ili kushughulikia malalamishi ya Wakenya kuhusu kuchelewesha kwa vyeti vyao vya kuzaliwa,” Matiang’i alisema.

Alisema kwama wizara yake itazidi kupiga kambi katika eneo hilo hadi mabadiliko katika huduma za vyeti vya kuzaliwa yatakapotimizwa.

“Tayari maafisa wawili katika afisi za CRB wamesimamishwa kazi na uchunguzi kuhusu kashfa za ufisadi dhidi yao kuanzishwa,” alisema

Ningali Nalia Nikiwa Chumbani Mwangu Nikimkumbuka Laboso, Abonyo Asema

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments