Makamanda wa kijeshi nchini Sudan waafikiana na upinzani

Waandamanaji nchini Sudan
Waandamanaji nchini Sudan
Baraza la jeshi nchini Sudan na muungano wa upinzani Jumatano waliafikiana kuhusu muongozo wa kugawaona mamlaka.

Maafikiano hayo yanalenga kuongoza juhudi za kuleta demokrasia nchini humo, kulingana na kituo cha televisheni nchini humo.

Makubaliano hayo yalitiwa saini mjini Khartoum chini ya uangalizi wa wapatanishi kutoka muungano wa Afrika. Hii ilikuwa baada ya majadiliano ya kina usiku kucha kujaribu kupata suluhu kwa maswala tata yaliokuwepo.

Habari zingine:

Baadhi ya makubaliano yalikuwa yameafikiwa mapema mwezi huu. Pande hizo bado zinaendelea na mikakati ya kupata muafaka kuhusu katiba huku stakabadhi za maafikiano zikitarajiwa kutiwa saini siku ya Ijumaa.