Makasiriko! Dadake Diamond Queen Darleen apewa block na mke mwenza

Dada yake msanii wa bongo Diamond Platnymz, Queen Darleen aliolewa mwaka jana Desember kama mke wa pili kwa mwanabiashara Isihaka Mtoro wawili hao walichumbiana kwa mwaka mmoja na kisha kuoana, huku mumewe akimwambia kuwa ana mke wa kwanza.

Msanii Darleen amesema kuwa hawajawahi onana ana kwa ana na mke wa kwanza wala kuzungumza naye, alikuwa anamuona kwenye mitandao ya kijamii na kwa sasa amempa block.

"Sajawahi onana naye wala kuzunguma naye nilikuwa na muoona kwenye mitandao ya kijamii lakini amenipa block, alinifuata kwenye mitandao ya kijamii kisha akaacha kunifuata kisha akanipa block."Alisema Darleen.

Darleen alisema kuwa mumewe angemuacha mkewe na kuenda kumtembelea walipokuwa wakichumbiana.

"Huwa nasema kuwa mume wangu ni wangu pekee kwa maana hatujawahi zungumzia mke huyo mwingine, lakini mume wangu huongea na mkewe."

Msanii huyo anatarajia mwanawe wa pili, huku akisema baba wa mtoto wake wa kwanza ni deadbeat.

"Wakati mtoto wangu alikuwa na miaka tatu tuliachana, hajui anavaa nini wala kula nini mimi ni baba na mama wa mtoto wangu ni mimi tu nimemsomesha mtoto wangu

Nikimuona sitamsalimia sina chuki wala kinyongo naye  lakini hajali kuhusu damu yake aliniahidi kumlea mtoto wangu lakini hakufanya hilo, niliumia."