Makubwa haya! Mhubiri West Pokot awalazimisha vijana kuabudu uchi

meme
meme

Mhubiri wa magharibi ya Pokot ametiwa mbaroni kwa kuwalazimisha watoto waache shule na kuenda kanisa lake ambapo yeye huwalazimisha waabudu wakiwa uchi.

Samwel Kalwsri ajiitaye Eliya alidai kuwa, aliamriwa na Mungu awache kazi yake na kuanza kumuabudu.

Kazi ya Samwel ni uuguzi lakini alisema kuwa Mungu ndiye aliyemwambia aache kazi yake na kumwabudu.

Zaidi ya hayo, amini usiamini, hata ikiwa Samwel ni muuguzi, huwa hawakubalii wafuasi wake kuenda hospitalini ikiwa wanaugua.

Jamaa huyu alitiwa mbaroni katika kitongoji cha waleteke.

Mke wake, Penina Lomatum alisema kuwa, mume wake alitoka nyumbani mwezi wa January mwaka wa 2017 kuenda kufanya kazi ya Mungu.

Mke wake, Lomatum alisema kuwa, jamaa huyu alikuwa anarudi nyumbani kila wiki kuwasalimia watoto wake lakini baada ya Januari mwaka wa 2017 hajarudi baada ya kupata mke mwengine.

''Tulipooana, nilimwambia siwezi enda kanisa lake na akaniwacha niende kanisa langu. Juzi juzi tu ndio nilijua kuwa ana jina jingine Eliya na ana mke mwengine.'' Mke wake alisema.

Vilevile, aliiambia serikali ifanye uchunguzi ili wahakikishe kuwa kanisa lake limeandikishwa kama kanisa katika orodha ya makanisa Kenya.

 Zaidi ya hayo, mke wake alisema kuwa,
''Nimesikia kuwa huwa hatumii chumvi na sukari na ata amekataa kutumia noti mpya za pesa. Niliskia pia amefungwa na ndio nikaamua nije kumsalimia.''Lomatum alisema.

Lomatum aliomba serikali imwachilie mume wake na kumruhusu arudi kwani hana kazi na alikuwa anategemea mume wake kukimu masomo na maisha ya watoto wake.
''Sina kazi na nilikuwa namtegemea akimu kila kitu cha familia. ''Mke wake alisema.

Mkubwa wa kitongoji kidogo cha Kipkomo bwana Mohammed Kofa alisema kuwa Kalwari alifungwa pamoja na wazazi wa watoto waliohusika.

''Tumemtia mbaroni mhubiri Samwel pamoja na wazazi wa watoto walioacha shule na kwa sasa, tunafanya uchunguzi ili tupate ujumbe zaidi kuhusu kanisa hilo na tujue ni nini haswa wao hufanya wakiwa wanaabudu uchi kule milimani.'' Kofa alisema.

Kofa aliwaomba machifu wa mtaa huo wahakikishe kuwa, watoto wote wanaenda shule na mzazi yeyote ambaye hampeleki mtoto wake shuleni ameshikwa na kufungwa.

''Wazazi ambao hawawapeleki watoto wao shuleni wanafaa kushikwa na kufungwa gerezani kwani ni haki ya kila mtoto kuenda shuleni kulingana na sheria.'' Kofa alisema.