Wanafunzi watatu wa shule ya upili ya wasichana ya Makueni wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Makueni kwa jaribio la kumuua mwenzao kwa kumwekea sumu kwenye chakula . watatu hao walio na umri wa miaka 15 na wa kidato cha Pili walipanga njama ya kutumia kemikali walizoiba katika maabara ya shule ili kumwua mwenzao anayemng’ng’ania mvulana mmoja wa shule jirani ya wavulana ya makueni .
Watatu waliokula njama ya kutekeleza mauaji hayo ni Beatrice Musomi ,Mercy wanjiku na Purity Akinyi ilhali aliyelengwa kuuawa ni mwenzao pia aliye na umri wa miaka 15 Faustine Kivuva. Watatu hao waliiba kemikali za phenolpthaline indicator, hydrochloric acid, benedicts solution ambapo Akinyi ndiye aliyefaa kuweka kemikali hiyo kwa chakula cha Kivuva .
Lakini njama hiyo ilitibuka wakati Ainyi aliposita kutekeleza wajibu wake na kumfanya Mercy Wanjiku kuripoti njama yao kwa kiranja wa darasa Brenda Keter ambaye baadaye alimfahamisha Naibu mwalimu mkuu Bi. Dorcas Nzioka. Mwalimu huyo ndiye aliyeripoti tukio hilo kwa polisi kuhusiana na tukio hilo ambalo limewatamausha wanafunzi wenzao na shule nzima ya wasichana ya Makueni .