Makumbusho ya 42 ya kifo cha hayati Mzee Kenyatta yafanyika faraghani

Kinyume  na makumbusho ya miaka ya awali ambapo makumbusho ya kifo cha hayati mzee Jomo Kenyatta yalifanyika hadharani huku viongozi mbali mbali wakialikwa mwaka huu mambo yalikuwa tofauti.

Soma habari zaidi;

Jumamosi Agosti 22 mwaka huu ilikuwa miaka 42 tangu mzee Kenyatta kufariki na hafla ya mwaka huu ilikuwa tofauti kwani ni familia ya marehemu hayati mzee Kenyatta pekee iliyohudhuria.

Hii pia ilikuwa mara ya kwanza rais Uhuru Kenyatta alikosa kuweka shada la maua katika kaburi la babake.

"Kama rais, nimeshauriana na familia ya Mzee Kenyatta. Tumekubaliana kwa pamoja kwamba makumbusho haya ya 41 yatakuwa ya mwisho kufanyika kwa njia hii," Uhuru alisema mwaka jana katika hafla iliyoandaliwa katika kanisa la Holy Family Basilica, Nairobi.

Soma habari zaidi;

Mzee Jomo Kenyatta alifariki Agosti 22, 1978 mwendo wa saa tisa unusu asubuhi akiwa usingizini katika Ikulu ya rais ya Mombasa.