Malava: Familia yadai haki baada ya jamaa yao kuuawa kinyama

Familia moja kutoka kijiji cha Chimoroni eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega inawataka maafisa wa usalama kuharakisha uchunguzi na kuwatia nguvuni wahusika wa mauaji ya jamaa yao.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 alibakwa na kisha kuuawa kinyama kwa kudungwa kisu, katika mtaa wa bahati kaunti jirani ya Uasin Gishu na watu wasiojulikana.

Kulingana na nduguye Alex Olindo, dadake Esther Olindo ambaye ana ulemavu wa kuongea, alikuwa akifanya kazi ya ususi mjini Eldoret, kabla ya kukumbana na mauti usiku wa tarehe 20 mwezi huu.