Malipo ni hapa duniani tu! Aliyetia chumvi na pili pili sehemu nyeti za mkewe atiwa mbaroni

James Kifo Muriuki ambaye aliwashangaza wengi baada ya kuibuka kuwa alimtia mkewe chumvi na pilipili katika sehemu zake nyeti na kufunga kwa kutumia glue ametiwa mbaroni akiwa mafichoni eneo la Kaningo kaunti ya Kitui.

Kupitia mtandao wa Twitter, DCI imesema kuwa kabla ya Muriuki kutekeleza unyama huo, alimtandika mkewe ndiposa akatekeleza uovu huo.

“She (the wife) was beaten by the suspect who also sprayed pepper, salt and super glue on her genitalia and later used a knife to push the said contents to her lady parts. Further, it was reported that he sealed her mouth and ears and left her for dead,”  DCI imesema .

Muriuki anadaiwa kuwa alimrusha mkewe katika mto Kathita na kumshinikiza kuvua nguo na kubaki uchi wa mnyama na kumlazimisha kuelezea wanaume ambao ameshiriki nao ngono akiwa jijini Nairobi.

Ni katika eneo hilo ambapo Muriuki anadaiwa kuwa alitekeleza unyama huo baada ya mwathiriwa kukataa kumjibu .

Taarifa zinasema kuwa Muriuki alitekeleza unyama huo huku mtoto wa miaka 3 mvulana akishuhudia kisanga hicho.

Majirani ambao walimsikia mtoto huyo akilia ndio waliomwokoa mwathiriwa na kumkimbiza hospitalini kupokea matibabu.

Afisi ya mpelelezi mkuu wa serikali DCI imesema kuwa Muriuki atashtakiwa pindi tu polisi watakapomaliza uchunguzi.