Malkia Strikers yafuzu awamu ya nusu fainali

Timu ya taifa ya voliboli upande wa wanawake, Malkia strikers ilifuzu kwenye awamu ya nusu fainali ya All African nations cup nchini Misri baada ya kuilaza Botswana seti tatu bila jibu.

Kwenye seti ya kwanza Kenya ililaza Botswana 25-16, seti ya pili ikashinda pia 25- 18 huku ikimaliza kazi kwa ushindi wa 25-11 kwenye seti ya tatu.

Awali, Malkia strikers ilikuwa imeilaza Algeria seti tatu bila jibu: 25-19,25-21 na 25-21. Malkia strikers sasa itamenyana na Cameroon kwenye mechi yao ya mwisho ya makundi huku ikiwa tayari imefuzu kwenye hatua ya nusu fainali.

Cameroon pia imefuzu kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mechi zake za kwanza mbili dhidi ya Botswana na Algeria mtawalia.Katika kundi A, Misri tayari imefuzu kwenye hatua ya nusu fainali.

soma pia

https://radiojambo.co.ke/zaeni-muijaze-tanzania-magufuli-awashauri-wanawake-wa-tz/