Malkia Strikers yasafiri hadi Japan kushiriki kombe la dunia

Timu ya kinadada ya voliboli nchini iliondoka jana kuelekea Japan ambapo wanatarajiwa kushiriki mashindao ya voliboli ya kombe la dunia, ya FVIB.

Timu hiyo chini ya ukufunzi wa kocha mkuu Paul Bitok imekua ikifanya mazoezi katika uwanja wa Kasarani, tangu kuregea kutoka kwa michuano ya All African Games ambapo walishinda nishani ya dhahabu. Malkia strikers watapambana na Marekani katika mechi yao ya ufunguzi siku ya Jumamosi kabla ya kuchuana na Uholanzi Jumapili.

Jumla ya timu 14 zimethibitisha kushiriki michuano ya mwaka huu ya raga ya Safari Sevens itakayoandaliwa kati ya tarehe 19 na 20 mwezi ujao. Mashindano hayo yatakua na timu 14 za kualikwa na timu mbili kutoka Kenya Shujaa na Morans.

Timu nne za ngazi ya juu bado hazijathibitisha iwapo zitashiriki lakini KRU inatarajia kupokea thibitisho lao kufikia wiki ijayo watakapoandaa kikao na wanahabari kutangaza timu zitakazoshiriki.

Soma mengi