Malumbano yashuhudiwa katika bunge la kaunti ya Nairobi: Rais kenyatta ahimizwa kuingilia kati

abdi
abdi
Wajumbe katika kaunti ya Nairobi wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kusitisha malumbano miongoni mwa wa wakilishi kutoka mrengo wa Jubilee.

Malumbano yalishuhudiwa katika mkutano uliofanyika siku ya jumatatu asubuhi kwani wajumbe hao walionekana kupigania cheo cha kiongozi wa wengi bungeni kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa na spika Beatrice Elachi wiki iliyopita.

 Juni Ndegwa ambaye ni mjumbe mteule alikuwa achukue nafasi yake Chege Waithera ambaye ni mjumbe eneo la South B, huku akisaidiwa na mjumbe wa Carlifonia Hassan Abdikadi.

Charles Thuo ambaye ni mjumbe katika eneo la Dandora 3 alikuwa achukue nafasi ya kiongozi wa wengi bungeni ambayo kwa sasa inashikiliwa na Abdi Guyo, huku Millicent Wambui ambaye ni mjumbe wa Ziwani alikuwa awe naibu wake.

Mabadiliko yaliyopendekezwa yalipingwa na wajumbe hao wakisema kuwa sio ya kikatiba.

Malumbano hizo zilianza katika ofisi ya kiongozi wa wengi mwendo wa saa tatu asubuhi, tukio ambalo liliwavutia maafisa wa usalama kufika katika eneo hilo.

Samuel Kobina ambaye ni afisa kutoka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai aliingilia kati na kuamuru wajumbe hao kuondoka katika mkutano huo masaa matatu baadaye.