Mama Ajishindia 'Ben ten' Migori

Shughuli za kawaida  zilisitishwa  mtaani  Oruba mjini  Migori baada ya wakaazi wa mtaa huo kumpata  mwanamke mwenye umri wa miaka 51  akiishi na mvulana  mwenye umri wa miaka 17  kama mume wake .

Kakake mvulana huyo  Erick Ochieng  amesema amekuwa akimtafuta  nduguye kwa muda  akidhani kuwa amepatwa na ajali anapoendesha boda boda yake.

Alishangaa kujulishwa na wenyeji kwamba mvulana huyo alikuwa akiishi na mwanamke huyo katika nyumba yake . Wenyeji waliokuwa na ghadhabu walimpa kichapo   mama huyo lakini alinusuriwa nma polisi .